Mshindi wa Maisha Plus 2012 kutoka Dar es salaam ni BERENIKI KIMIRO, amejishidia Tshs.
Millioni 20.
BERENIKI KIMIRO alianza kwa Kumshukuru Mungu kwa
ushindi, amsema ye si kitu kwa wenzake, hilo ni zali tu.. Amemshukuru
baba yake mzazi kwa kumshauri kusali. Aliwashukuru pia wapenzi
watazamaji kwa kumpiga kura, ameahidi kuendeleza kile alichokianzishaa
kijijini na kuitendea haki nchi yake
Alimshukuru babu, Brother Masoud
na Crew nzima ya Maisha Plus.. Alimshukuru pia mwanae Kelvin (6yrs) kwa
kuvumilia kipindi chote bila kuongea na mama. Alisema Mungu amejibu
maombi yake kwani ukipiga goti, maombi yako yatajibiwa..
Mshindi wa Pili ni Venance Mushi kutoka Dodoma amejishindia Tshs.
Million 6.

Mshindi wa Tatu ni Justine Bayo, kutoka Morogoro amejishindia Tshs. Million
4.
Naibu
Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu aliitwa kusema
machache pamoja na kutangaza Mshindi wa Maisha Plus 2012.. Masoud
Kipanya, alimkaribisha, akishukuru kwa zawadi aliyoitoa ya ya Tshs.
Millioni 10 ambayo itagawanyika Millioni 6 kwa Mshindi wa Pili na
Million 4 kwa mshindi wa tatu.
Mhe.
Nyalandu aliongezea zawadi ya Tshs. Million 7.5 ili igawanywe Tshs.
Laki tano kwa kila mshiriki ambaye hakuingia top 3, aliwakaribisha pia
washiriki wote kwa chakula cha Mchana siku ya kesho katika hoteli ya
Serena.
No comments:
Post a Comment